Wakati nyota ikiishiwa mafuta, wanaastronomia husema kuwa imefika mwisho wa maisha yake, ingawa wanachokimaanisha ni kuwa imefika mwisho wa maisha yake ya kawaida. Wanaastronomia huiita hii ya kuishiwa mafuta kuwa ni kipindi muhimu cha nyota, ila kama huu sio mwisho wa nyota je ni nini kinachotokea baadae?
Kinachofuta mara nyingi hutegemeana na uzito wa nyota husika. Kwa nyota zenye uzito mkubwa maisha yanayofuata ni ya kutatanisha sana kwani huwa zinalipuka! milipuko iitwayo ‘Supanova’ na wanaastronomia. Milipuko hiyo mara nyingi hutengeneza maumbo ya kupendeza- kama vipepeo wa kupendeza wanaotoka katika pupa na wanaastronomia huita maumbo haya mabaki ya supanova.
Angalia katika picha utaona rangi na sura nzuri ya baki la supanova. Maumbo kama haya sio tu kwamba yanapendeza lakini pia yanapoangaliwa kwa ukaribu, kwa mfano nyota iliyolipuka katika mfumo wa supanova hutoa mwanga mwingi kama ule wa galaxi nzima ambayo ina nyota zaidi ya mabilioni.
Lakini bado kwani ni kiasi kidogo tu cha taarifa kuhusu ni jinsi gani supanova inatokea ndio tunajua, hivyo kuisoma nyota kabla haijalipuka na kuwa maarufu ulimwenguni kote! kutaweza kuwapa wanaastronomia vidokezo muhimu kuhusiana na milipuko hii.
Kwa sasa timu ya wanaastronomia wamesema kwa uhakika kile wanachofikiri kuwa wamekifanya na kama uvumbizi wao utathibitishwa, basi hii itakuwa ni supanova ya kwanza kugunduliwa kabla ya kulipuka.
Dokezo
Wakati wa mlipuko wa supanova, maada kutoka katika nyota hutupwa nje katika mwendo kasi mkubwa sana unaokaribia 30,000 km kwa sekunde! Hiyo ni takribani ya mara 10 chini ya mwendo wa mwanga!
Share: